MWAMUZI MISRI AFUNGIWA KWA KUWAPONDA EFA
Chama cha soka cha Misri (EFA) kimemsimamisha mwamuzi Saeed Hamza kwa miezi mitatu baada ya kuonekana kukikosoa chama hicho kwenye Televisheni.
Hamza alionekana katika TV bila ya kutoa taarifa kwa EFA, akiwakosa EFA na kamati ya waamuzi kwa kushindwa kuwalipa pesa zao.
EFA tayari wameanza kufanya uchunguzi juu ya mwamuzi huyo na jana Jumatatu walimuita makao makuu na akaomba msamaha kwa kamati ya EFA na CEO kwa alichokisema.
Hamza alilalamika kuhusu waamuzi kutolipwa kwa miezi saba iliyopita, na pia aliwakosoa EFA kwa kutowapa waamuzi vifaa vipya vya kazi na nguo licha ya kutumia Egypty Pounds Milioni 80 (Tsh Bilioni 11.7) katika kuleta VAR kwenye ligi ya kuu ya Misri.