MANE YUPO TAYARI KWA LOLOTE KUHUSU UBINGWA
Nyota wa klabu ya Liverpool Sadio Mane ameweka wazi msimamo wake kuhusu ubingwa wa ligi kuu nchini England ambao wanaufukuzia na kukaribia kuupata baada ya kuukosa ndani ya miaka 30.
Kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu kuendelea kwa msimu au kufutwa kutokana na uwepo wa virusi vya Corona ambavyo vimepelekea kusimama kwa ligi nyingi duniani ili kujilinda dhidi ya maambukizi.
Bado haijawa wazi kama itaamuliwaje kuhusu ubingwa kama msimu utasitishwa, Mane akisema kuwa hatafurahia kama watapewa ushindi wa mezani ila anataka ubingwa kwa kucheza uwanjani.
Hata hivyo Msenegal huyo anasisitiza atakubali maamuzi yoyote yatakayofanywa hata kama ni kukosa ubingwa kabisa.
“Chochote kitakachotokea nitaelewa. Imekuwa ngumu kwa Liverpool, lakini imekuwa ngumu zaidi kwa mamilioni ya duniani kote.” Sadio Mane alizungumza katika mahojiano na talkSPORT.