UFC KUENDELEA KAMA KAWAIDA
Raisi wa mchezo wa UFC Dana Whie maesema mchezo huo utaendelea kama kawaida na kwa sasa wapo mbioni kupata kisiwa binafsi cha kuhodhi mchezo huo katika kipindi hiki cha mlipuko wa corona.
Akizungumza na jarida la TMZ White amedai mchezo huu utaendelea tena April 18 baada ya shirikisho la mchezo huo kulazimika hairisha matamasha matatu hivi karibuni kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
Kutokana na baadhi ya nchi kuweka zuio la kusafiri White amepanga kutumia kisiwa hicho kama sehemu ya kuepuka masharti hayo kwa kutumia ndege binafsi kuwasafirisha wapiganaji kwenda kisiwan humo. Bingwa wa lightweight Khabib Nurmagomedov alitakiwa pigana na Tony Ferguson jijini New York kwenye UFC 249 ila kutokana na kuwepo katika karantini nchini Russia, Justin Gaethje atachuua afasi yake.
Whote alisema wapiganaji watapimwa kila wakati na ngumi hazitakuwa na mashabiki kwani watahakikisha kila mmoja nakuwa salama dhidi ya virusi vya corona kabla na baada ya ngumi.