LIGI KUU UJERUMANI KUREJEA BILA MASHABIKI
Ligi Kuu ya nchini Ujerumani (Bundesliga) inawezekana ikawa Ligi ya kwanza Ulaya kurejea na kuanza kuchezwa mwezi Mei baada ya wachezaji wa vilabu shiriki kuanza mazoezi.
Mtendaji mkuu wa Bundesliga Christian Seifert amethibitisha hilo leo kuwa Ligi itarejea lakini bila uwepo wa mashabiki uwanjani kuanzia mwezi Mei kwa msimu mzima baada ya kusimama kwa sababu ya corona.
Hata hivyo hadi sasa nchini Ujerumani jumla ya vilabu 36 vya soka vya Ligi Kuu na madaraja mengine vimeanza mazoezi yake hali ambayo imekuwa kiashiria kizuri kuwa Bundesliga inarejea karibuni.