APP YA AFYA KURUDISHA LIGI YA ENGLAND NA MASHABIKI
Pengine tunaweza kushuhudia ligi kuu nchini England ikarejea kuchezwa pamoja na mashabiki kama mambo yataenda sawa kutokana na ligi hiyo kuanza kuijarabu Programu (App) ambayo itakuwa inaruhusu tiketi za mechi kuuzwa kwa watu ambao hawana maambukizi ya virusi vya Corona
Kampuni ya teknolojia ya Uingerexa iitwayo VSTE imetengeza App hiyo ambayo inatoa Pasipoti ya afya (Health Passport) ambayo inaweza kuonesha mtu ambaye amepimwa na kukutwa hana virusi vya Corona au mwenye kila mwili zinazompa kinga.
Vipimo vya afya vitaendelea kufanywa na kusimamiwa na wataalamu wa afya na matokeo ya vipimo hivyo ndio yataingizwa kwenye App hiyo inayoitwa V-COVID digital health passport.
Inaelezwa kuwa serikali ya Uingereza tayari ipo kuitafiti App hiyo ikiwa ni njia ya kulisaidia shirika lao la afya (NHS) katika kuwezesha watu wanaweza kurudi makazini.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, Mtendaji Mkuu wa ligi kuu ya England Richard Masters anajiandaa kukutana na watengenezaji wa APP hiyo VST Enterprises (VSTE) wiki hii ili kujua inatumikaje kuangalia afya za mashabiki wanaoingia uwanjani.