CANADIAN GRAND PRIX ZAWA MBIO ZA 9 KUHAIRISHWA FORMULA 1
Zikiwa ndio mbio zilizotarajiwa kuanza kwa msimu huu baada ya kushindikana kuanza kwa mbio zozote tokea mwanzoni mwa mwaka kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, mbio za Canadian Grand Prix ‘Montreal’ zilizokuwa zifanyike trehe 14 Juni nazo zimehairishwa huku waandaaji wakihaidi kutaangalia uwezekano wa kufanya mbio hizo hapo baadae mwaka huu.
Formula 1 wanafaya jitihada za kuona kila wezekanowa kufayika kwa mbio 8 tu kati ya 22 mwaka huu ambazo ndio kiwango cha chini cha mbio kinachohitajika ili kuweza pata msindi huku hadi sasa mbio 9 zikiwa zimehairishwa na moja kufutwa.
Mbio inayofuata ambayo bado ipo kwenye ratiba baada ya hizi ni zile za Austria Grand Prix ambazo zinatarajiwa fanyika Julai 5, zikiwa na matumaini baada ya nchi hiyo kuwa ya kwanza barani Ulaya kulegeza zuio la kusafiri huku mikusanyiko na matamasha yakiwa bado yamezuiliwa mpaka mwishoni mwa mwezi Juni.
Mbio za Canadian Grand Prix msimu uliopita 2019 zilimalizika kwa Lewis Hamilton kushinda mbio hizo baada ya hasimu wake Sebastian Vettel kupigwa penati ya sekunde 5 kwa kosa la kungia vibaya kwenye mzunguko jambo ambalo alipinga na kulaamika kuwa alipokwa ushindi na viongozi wa mbio hizo.