MOURINHO HANA UHAKIKA NA DE GEA
Kocha wa Man United Jose Mourinho hana uhakika kama kipa David De Gea atasaini mkataba mpya klabuni hapo.
Mhispania huyo amejitambulisha kuwa moja ya makipa bora duniani tangu atue Old Trafford akitokea Atletico Madrid mwaka 2011, akishinda tuzo ya mchezaji bora ya mwaka wa klabu hiyo mara nne katika misimu mitano iliyopita.
De Gea alikuwa akihusishwa na kuhamia na Real Madrid, lakini uhamisho wake ulifeli baada ya kusaini mkataba mpya ambao utaisha mwaka 2019 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.
Uhamisho wa majira ya kiangazi wa Thibaut Courtois uliongeza matumaini ndani ya klabu ya Man United kuwa De Gea atakubali kusaini mkataba mpya, lakini Jose Mourinho hana uhakika na mustakabali wa kipa huyo ambaye kwa sasa anahusishwa na kujiunga na mabingwa wa Italy, Juventus.
‘Sina hakika‘ Jose aliiambia Sky Sports alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo kusaini mkataba mpya.
‘Lakini pia sina wasiwasi. Tusubiri tuone nini kinatokea. Ni klabu pekee, David na watu wake David, wanaweza kujibu swali hilo.
‘Maoni yangu ni kila mmoja anajua ni jinsi gani ni mzuri, kila mtu anajua alivyo na umuhimu kwa Man United.
Na kama Manchester United wanataka kuwa bora zaidi walivyo sasa na kutokuwa vibaya zaidi walivyo sasa, ni wazi kwamba itakuwa ni lazima kumbakisha David‘