GAUCHO ATOLEWA JELA PARAGUAY
Nyota wa zamani wa Barcelona na Brazil Ronaldinho Gaucho pamoja na kaka yake wameachiwa kutoka jela huko Paraguay baada ya kulipa dhamana ya Dola Milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7)
Wawili hao wamekaa jela kwa muda wa siku 32 baada ya kukamatwa kuingia nchini Paraguay na Passport bandia na wanakabiliwa na hukumu ya miezi sita jela.
Ronaldinho pamoja na kaka yake sasa wamewekwa chini ya ulinzi katika hoteli iliyopo mji mkuu wa Paraguay,Asuncion
Jaji Gustavo Amarilla amewapa ruhusa ya kukaa hotelini kwa muda huu ambao kesi bado haijafikiwa maamuzi, huku wanasheria wa mchezaji huyo wakijaribu kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya kifungo cha jela.