MADEREVA WA TIMU ZA WILLIAMS NA RACING POINTS WAPUNGUZIWA MISHAHARA
Timu za Racing Point na Williams zimechukua hatua ya kupunguza sehemu za wafanyakazi wao na kuwapa likizo za lazima ikiwa ni pamoja na kuwakata mishahara madereva wao kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. Hatua hii imekuja baada ya wiki iiyopita timu ya McLaren kuchukua hatua kama hii.
Timu ya Williams imesema kiasi cha wafanyakazi wao watachukua likizo za lazima mpaka mwishoni mwa mwezi Mei huku madereva George Russell na Nicholaus Latifi pamoja na viongozi waandamizi wakiwa wameanza katwa asiimia 20 ya mishahara yao tokea Aprili 1.
Upande wa Racing Point wamesema madereva Sergio Perez na Lance Sroll motto wa billionea na mmiliki wa timu hiyo Lawrence Stroll watapunguziwa mishahara kwa hiari huku wafanyaazi wengine wakichukua likizo za lazima kutokana na hali kuendelea kuwa mbaya.
Timu hizi mbili zenye makazi yake Uingereza zimefikia hatua hii baada ya kikao cha mabosi wa timu za Formula 1 siku ya Jumatatu kilichokuwa mahususi kwa ajili ya kutafuta njia zakuunusuru mchezo huu ambao umeendelea kupata hasara kutokana na kutofanyika kwa mbio.