NIGERIA IMEMPA OFA YA MKATABA MPYA KOCHA KWA MASHARTI
Shirikisho la mpira wa miguu nchini Nigeria (NFF) limetoa masharti mazito kwa kocha wake mkuu Gernot Rohr kuwa ipo tayari kumpa mkataba mpya kwa masharti.
NFF limempa ofa Rohr raia wa Ujerumani ya kuendelea kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria “Super Eagles” ila kwa masharti makuu mawili juu ya makazi yake na mshahara wake.
Rais wa NFF Mr Amaju Pinnick ametangaza kuwa ni kweli wamempa ofa ila kwa masharti ya kutaka makazi yake yawe ndani ya Nigeria pili awe analipwa mshahara wake kwa Naira (Pesa ya Kinigeria) sio kwa dola au pesa yoyote ya kigeni kama ilivyokuwa awali.
Rohr ni kocha wa timu ya taifa ya Nigeria toka 2016 na mkataba wake wa sasa unamalizika Julai 2020, lengo kuu la kutaka akae ndani ya Nigeria ni kutokana na kutaka awe na nafasi ya kusafiri mikoa mbalimbali ya Nigeria ili kuona mechi za Ligi Kuu ya isimpe tabu kuita kikosi kama atahitaji wachezaji.