Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri ambaye yupo nchini Misri, jana ametembelea kambi ya Taifa Stars na kuwatia moyo wachezaji wa timu hiyo huku akiwataka wasikate tamaa. Nahodha Mbwana Samatta ambaye pia amejenga Kigamboni amemkabidhi DC Sara jezi ya timu ya Genk anayochezea . DC Sara yupo Misri kuiunga mkono Taifa Stars ambayo itacheza …
Read morePato aondoka Yanga na kutua Polisi
Kiungo Mkabaji aliyekuwa katika Klabu ya Yanga Pato Ngonyani, amejiunga na Polisi Tanzania FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Read moreSamatta ajiunga na KMC
Kiungo mshambuliaji Mohamed Samatta amejiunga na klabu ya KMC akitokea Mbeya City kwa mkataba wa miaka mitatu. Huyu ni kaka wa mshambuliaji wa Genk na Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta.
Read moreMsolla awapa onyo wanautumia nembo ya Yanga vibaya
Klabu ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wa Klabu hiyo Mshindo Msolla imewatak wale wote wanaotumia nembo ya Yanga kutengeneza jezi wafike makao makuu ya Klabu hiyo ili waweze kufanya mazungumzo. Msolla pia amewataka wale wanaotumia mitandao ya kijamii kwa jina la Klabu ya Yanga waache tabia hiyo maana klabu hainufaiki chochote kupitia mitandao hiyo .
Read moreMbrazil mwingine atua Simba
Klabu ya Simba SC imemsajili beki Tairone Santos da Silva raia wa Brazil kwa mkataba wa miaka miwili. Da silva,30, amejiunga na klabu hiyo akitokea Atlético Cearense FC ya nchini Brazil.
Read moreKapombe amwaga wino Simba
Bek wa kulia anayecheza Klabu ya Simba Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea Klabu hiyo. Kupitia ukurasa wa instagram ya Klabu ya Simba SC umeandika kuwa Kapombe kwa sasa yupo fiti kucheza na atakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitaenda nje ya nchi kujiandaa na msimu mpya baada ya kuwa nje …
Read moreMwanamitindo amponza nyota wa Misri
Uongozi wa timu ya taifa ya Misri mapema jana kabla ya mchezo na DR Congo walifikia maamuzi ya kumuondoa kikosini nyota wao Amr Warda. . Warda anayekipiga PAOK ya Ugiriki anaondolewa katika kikosi cha AFCON cha Misri baada ya kucheza mchezo mmoja, hiyo ni baada ya mwanamitindo mwenye asili ya Misri na Uingereza Merhan Keller …
Read moreKotei asajiliwa Keizer Chiefs
Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imemsajili kiungo James Kotei kutoka Simba kwa mkataba wa miaka mitatu Kotei alikuwa ni mshindi wa tuzo ya kiungo bora wa Simba katika msimu uliomalizika.
Read moreJackson Mayanja atua KMC
Baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Klabu ya KMC Etienne Ndayiragije kuondoka na kujiunga na Klabu ya Azam, KMC imemnasa aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Klabu ya Simba SC Jackson Mayanja kwa mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Klabu hiyo. Uongozi wa KMC kupitia kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amesema kuwa wanaimani …
Read moreMakonda atua Misri kutoa hamasa kwa Stars
Mwenyekiti wa Kamati ya uhamasisha ya Taifa Stars taifa,mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewasili nchini Misri kwa ajili ya kuendelea kuipa hamasa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Makonda amesema kuwa wao walioenda nchini Misri wameenda na matumaini makubwa ya kwamba Taifa Stars inaweza na wachezaji watafanya vizuri kadri ya …
Read more