PSG, Juventus na Real Madrid zazidi kuipa Presha Chelsea
Kiungo wa kibelgiji Eden Hazard bado anaendelea kuipasua kichwa Chelsea ambayo inahaha kumshawishi aongeze mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendeleakutoa huduma Stamford Bridge chini ya Kocha mkuu wakikosi hicho Maurizio Sarri. Kutokana na Hazard kutoonekana msimamo wake wamoja kwa moja, kwa sasa unaweza kusema yupo mguunje mguu ndani, Chelsea wanatajwa kuandaa dau zitolitakalombakiza nyota huyo Uingereza na kufuta mawazoya kwenda Hispania ambako amekuwa akihusishwa napomara kwa mara. Chelsea wakiwa wamemuwekea ofa ya mshahara wapauni 300000 kwa wiki, ushindani wa timu kuwaniasaini ya mchezaji huyo umeongezeka kufuataia klabu zaJuventus, PSG na Real Madrid kumuhitaji ila Real Madrid wanatajwa kuja kwa kasi zaidi kuhitaji saini yanyota huyo. Kikubwa kinachoipasua kichwa Chelsea ni kutokana nanyota huyo wa kibelgiji yupo mbioni kumaliza mkatabawake mwisho wa msimu, hivyo klabu zinaisukumaChelsea ili imuuuze Januari katika majira ya usajili yadirisha dogo, hata hivyo Hazard alikuwa sehemu ya timuya Chelsea iliyovunja rekodi ya Manchester City kutopoteza mchezo 21 ya Ligi Kuu mfululizo.
Read more