Refa wa Kenya kuandika rekodi mpya leo AFCON
Peter Waweru anataraji kuwa mwamuzi wa kati wa kwanza kutoka Kenya kuchezesha mechi ya AFCON. Waweru ambaye ni mhadhiri katika chuo cha JKUAT (Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology) amechaguliwa na CAF kuchezesha mechi ya kundi D kati ya Namibia na Ivory Coast itakayochezwa leo saa moja kamili usiku.