De Ligt atua rasmi Juventus
Klabu ya Juventus leo wametangaza rasmi kumsajili beki wa kati Matthijs de Ligt kutoka Ajax kwa ada inayoripotiwa kuwa Pauni Milioni 67.5 sawa na Tsh Bilioni 193. Mholanzi huyo,19, amesaini mkataba wa miaka mitano
Klabu ya Juventus leo wametangaza rasmi kumsajili beki wa kati Matthijs de Ligt kutoka Ajax kwa ada inayoripotiwa kuwa Pauni Milioni 67.5 sawa na Tsh Bilioni 193. Mholanzi huyo,19, amesaini mkataba wa miaka mitano
Shirikisho la soka la Afrika CAF limefanya mabadiliko ya mwamuzi wa mechi ya fainali ya AFCON 2019 kati ya Senegal na Algeria zikiwa zimepita saa 24 tangu wamtangaze mwamuzi wa Afrika Kusini Victor Gomes kuwa ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Shirikisho hilo sasa limemtangaza Mwamuzi Neant Alioum kutoka Cameroon kuwa ndiye atakayeshika filimbi hapo kesho. Mwamuzi …
Atletico Madrid wametangaza kumsajili beki Muingereza Kieran Trippier kutoka Tottenham kwa ada ya Pauni milioni 21.7 Trippier,28, anakuwa ni Muingereza wa kwanza kuichezea Atletico Madrid ndani ya miaka 95.
Baada ya kuonekana amepaka rangi nywele zake, nyota Mesut Ozil ameeleza sababu iliyofanya afanye hivyo. Kiungo huyo amesema alipoteza bet ya kugongesha mwamba (crossbar challenge) dhidi ya mchezaji mwenzake wa Arsenal Alexandre Lacazette hivyo ikambidi atimize ahadi.
Ikiwa mabadiliko katika sekta mbalimbali yanaendelea ndani ya Klabu ya Yanga Mwenyekiti wa klabu hiyo Mshindo Msolla amesema kuwa Kocha mkuu Mwinyi Zahera amemchagua Kocha Noel Mwandila kuwa msaidizi wake kwa kuwa anavigezo vyote vya kuwa katika nafasi hiyo. Msolla kupitia Clouds FM amesema Kocha Zahera atafanya mabadiliko katika Benchi la ufundi lakini Kocha Mwandila …
Baada ya jana uongozi wa Klabu ya Simba kupitia kwa Mkurugenzi wake Crescentius Magori kusema kuwa haimtambui aliyekuwa mdhamini wa Klabu hiyo Mzee Hamisi Kilomoni kama mdhamini ndani ya Klabu hiyo tangu mwaka 2017 walipomvua wadhifa huo,na kuamua kumpeleka kwenye Kamati ya maadili ya TFF na kumshtaki kwa kosa la kupotosha umma kuwa yeye bado …
Uongozi wa Klabu ya Simba kumshitaki beki wake wa kati Juuko Murshid kwa kosa la kutorudi kwenye timu yake na kuendelea na majukumu yake. Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Crescentius Magori amesema kuwa mchezaji huyo aliitwa na uongozi wa klabu lakini hakuweza kufika hivyo wameamua kumshitaki kwenye Kamati ya maadili ya TFF. Magori amesema kuwa …
Mbrazil Neymar Jr amesisitiza nia yake ya kutaka kuondoka PSG baada ya kufanya kikao kifupi na Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Leonardo, wameripoti ESPN. Neymar anahusishwa na kutaka kurejea katika timu yake ya zamani ya Barcelona aliyoihama mwaka 2017 na kwenda PSG kutaka kutengeneza ufalme wake.
Kiungo Fabian Delph amesajiliwa na klabu ya Everton kutoka Man City kwa ada ya awali Pauni milioni 8.5, na kusaini mkataba wa miaka mitatu. Muingereza huyo ,29, na Everton baada ya kuitumikia Man City kwa muda wa miaka minne.
Baada ya mkataba wa aliyekuwa Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Amiss Tambwe kumalizika,mchezaji huyo ameweka wazi kuwa uongozi haukutaka kumuongezea mkataba kutokana na Kocha Zahera kutokumuhitaji. Tambwe kupitia EFM radio amesema kuwa Kocha mkuu wa Yanga amewaacha wachezaji wengi wazuri lakini hawezi kujua mipango yake ni ipi. . “Kama Kocha hakutaki kulingana na mipango yake …