Pato aondoka Yanga na kutua Polisi
Kiungo Mkabaji aliyekuwa katika Klabu ya Yanga Pato Ngonyani, amejiunga na Polisi Tanzania FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kiungo Mkabaji aliyekuwa katika Klabu ya Yanga Pato Ngonyani, amejiunga na Polisi Tanzania FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kiungo mshambuliaji Mohamed Samatta amejiunga na klabu ya KMC akitokea Mbeya City kwa mkataba wa miaka mitatu. Huyu ni kaka wa mshambuliaji wa Genk na Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta.
Klabu ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wa Klabu hiyo Mshindo Msolla imewatak wale wote wanaotumia nembo ya Yanga kutengeneza jezi wafike makao makuu ya Klabu hiyo ili waweze kufanya mazungumzo. Msolla pia amewataka wale wanaotumia mitandao ya kijamii kwa jina la Klabu ya Yanga waache tabia hiyo maana klabu hainufaiki chochote kupitia mitandao hiyo .
Klabu ya Simba SC imemsajili beki Tairone Santos da Silva raia wa Brazil kwa mkataba wa miaka miwili. Da silva,30, amejiunga na klabu hiyo akitokea Atlético Cearense FC ya nchini Brazil.
Bek wa kulia anayecheza Klabu ya Simba Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea Klabu hiyo. Kupitia ukurasa wa instagram ya Klabu ya Simba SC umeandika kuwa Kapombe kwa sasa yupo fiti kucheza na atakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitaenda nje ya nchi kujiandaa na msimu mpya baada ya kuwa nje …
Uongozi wa timu ya taifa ya Misri mapema jana kabla ya mchezo na DR Congo walifikia maamuzi ya kumuondoa kikosini nyota wao Amr Warda. . Warda anayekipiga PAOK ya Ugiriki anaondolewa katika kikosi cha AFCON cha Misri baada ya kucheza mchezo mmoja, hiyo ni baada ya mwanamitindo mwenye asili ya Misri na Uingereza Merhan Keller …
Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imemsajili kiungo James Kotei kutoka Simba kwa mkataba wa miaka mitatu Kotei alikuwa ni mshindi wa tuzo ya kiungo bora wa Simba katika msimu uliomalizika.
Baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Klabu ya KMC Etienne Ndayiragije kuondoka na kujiunga na Klabu ya Azam, KMC imemnasa aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Klabu ya Simba SC Jackson Mayanja kwa mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Klabu hiyo. Uongozi wa KMC kupitia kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amesema kuwa wanaimani …
Mwenyekiti wa Kamati ya uhamasisha ya Taifa Stars taifa,mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewasili nchini Misri kwa ajili ya kuendelea kuipa hamasa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Makonda amesema kuwa wao walioenda nchini Misri wameenda na matumaini makubwa ya kwamba Taifa Stars inaweza na wachezaji watafanya vizuri kadri ya …
Baada ya kuwa na maneno ya kuwakatisha tamaa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ baada ya kufungwa goli 2-0 dhidi ya Senegal Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limewataka watanzania kuendelea kuiunga mkono na sio kuivunja moyo timu hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa TFF uliopo Ilala Karume …