Nicklas Bendtner ahukumiwa jela
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner amehukumiwa jela kwa muda wa siku 50 kwa kosa la kumshambulia dereva wa taxi. Mdenmark huyo,30, anayecheza Norway katika klabu ya Rosenborg amekataa rufaa dhidi ya hukumu hiyo. Pia mahakama imemtaka mchezaji huyo kumlipa dereva huyo pauni 1000 ( Tsh Milioni 2.9) Kama fidia. Bendtner alivunja taya ya …