LIVERPOOL WAGOMA KURUDISHA FEDHA KWA ATLETICO
Klabu ya Atletico Madrid imeamua kuwalipa fidia mashabiki 290 ambao hawakusafiri kwenda Anfield kwa katika mechi ya marudiano klabu bingwa dhidi ya Liverpool kwa hofu ya virusi vya Corona.
Ripoti zinasema kuwa Atletico wameamua kufanya hivyo baada ya Liverpool kukataa kurudisha fedha yoyote.
Kwa mujibu wa gazeti la Hispania AS, Atletico wamerudisha kiasi cha Pauni 15,000 (Tsh milioni 42.8) kwa mashabiki hao ambacho walikitumia kununua tiketi.
Ripoti zinasema Liverpool walichukua mapato ya tiketi hizo za mashabiki hao 290 na kugoma kurudisha.
Mechi hiyo ya marudiano iliyopigwa Machi 11 iliisha kwa Liverpool kupoteza kwa goli 3-2, Atletico wakifuzu robo fainali kwa jumla ya goli 4-2.