JURGEN KLOPP KUONGOZA JOPO LA MAKOCHA KUKATWA MISHAHARA EPL
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp na kocha wa West Ham United David Moyes ni miongoni mwa makocha wa Ligi Kuu nchini England walioridhia kukatwa mishahara yao wakati huu wa virusi vya corona.
Wachezaji wa Liverpool wakiongozwa na Jordan Henderson wapo radhi kukatwa mishahara yao lakini wanataka iende katika mifuko na taasisi zitakazosaidia mapambano dhidi ya virusi vya corona na sio wakatwe halafu ibakie katika klabu.
Wengi wao wanataka pesa hizo ziende katika mfuko wa NHS (National Health Service) utakaosaidia katika kutoa huduma za afya kwa waathirika wa virusi vya corona.
Inaripotiwa kuwa makocha wa EPL wapo upande wa vilabu kukubali kukatwa mishahara yao, hadi kufikia asubuhi ya leo April 6 2020 Uingereza ilikuwa na vifo 4934 vilivyotokana na corona.