WACHEZAJI LIGI BARA WAKATAZWA KUSALIMIANA KWA MIKONO
Katika kujilinda na virusi vya Corona, TFF imetangaza kuanzia leo hakutakuwa na utaratibu wa wachezaji kusalimiana kwa mikono kabla ya mechi kuanza na badala yake watatumia ishara. Hii imekuja baada ya Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu kutangaza kuwa watu wasisalimiane kwa mikono ikiwa ni njia ya kuchukua tahadhali dhidi ya virusi hivyo.