WACHEZAJI NA WAKURUGENZI WA BAYERN NA DORTMUND KUKATWA MISHARA
Baada ya ligi ku ya nchini Ujerumani Bundesliga kusimama kwa tokea tarehe 8 mwezi Machi kutokana na mlipuko wa virusi ya corona, wachezajina wakurugenzi wa timu za Dortmund na Bayern wamekubali kukatwa mishahara yao ili kusaidia klaby kuweza mudu gharama za kulipa wafanyakazi wengine.
Bayern wakikatwa asikimia 20 ya mishahaa yao , Dortmund watajitolea kiasi cha mishahara. Hatua hii inakuwa muendelezo wa wachezaji kujitoa katika kipindi hiki kigumu baada ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Union Berlin kutangaza hawatapokea kabisa mishahara kipindi hii kutokana na hali mbaya iayoendelea huku wakiwa hawajui ni hadi lini wataendelea na hali hii.
Wiki iliyopita wachezaji wa Borussia Monchegladbach walikuwa wa kwanza kutangaza hawatopokea mishahara kabisa ikiwa ni njia moja wapo ya wao kusaidia hali katika kipindi hiki.
Wiki iliyopita mshambuliaji Robert Lewandoski na mkewe Anna walichagia kiasi cha yuro millioni 1 (Takribani shilling billion 2.3) kwa ajili ya kupambana na janga hii.
Siku ya Jumatano mamlaka ya nchini Ujerumani iitangaza kufikia kesi 31,554 za corona nchini humo na vifo 149