KLABU YA YANGA IMESIMAMISHA WAJUMBE WAWILI
Klabu ya Yanga wakati kukiwa katika heka heka za kumrudisha mdhamini wao GSM ambaye amekuwa akijitolea kupita kawaida leo imetangaza maamuzi magumu.
Yanga leo imetangaza rasmi kuwasimamisha wajumbe wake wawili wa kamati ya utendaji Salum Rupia na Franka Kamugisha kwa tuhuma za kinidhamu.