KIUNGO WA AJAX AZINDUKA BAADA YA KUWA KATIKA COMA MIAKA 2
Baada ya nyota wa Ajax ya nchini Uholanzi Abdelhak ‘Appie’ Nouri kuanguka na kupoteza fahamu uwanjani July 2017 kwa tatizo la moyo (cardiac arrhythmia) katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Werder Bremen.
Leo mtandao wa ad.nl umeongea na kaka wa mchezaji huyo na ameeleza kuwa Nouri amezinduka na fahamu kumrejea baada ya kuwa katika coma kwa miaka miwili na miezi 9.
Kwa mujibu wa kaka yake wa damu Nouri ameanza kuleta matumaini kwa kuwa na uwezo wa kuchezesha baadhi ya viungo vya mwili wake kama macho, sura na kuwa na uwezo wa kula.