“BORA MIMI NIONDOKE, GSM ABAKI”
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga SC Shija Richard leo hii ametangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo kwa kile alichokiita maslahi mapana ya klabu hiyo.
Shija kupitia Azam TV ameeleza kuwa ipo sababu iliyomfanya ajiuzulu kuhusiana na malumbano na mdhamini wao GSM lakinii hawezi kuweka wazi kwa sababu haoni haja ya kufanya hivyo italeta malumbano.
”Nimejiuzulu kwa sababu Yanga ni kubwa kuliko mimi, pamoja na kuwa tunadhaminiwa tunapewa fedha lakini kuna maswala ambayo yanayakiwa kufanyika na kamati ya utendaji na kuna maswala yanatakiwa yafanyike na mdhamini”
”Msipokuwa na mipaka ya utendaji wa kazi mambo yanaweza yakaenda Shaghalabaghala sasa katika kipindi hiki kuliko kuendeleza malumbano nikafikiri mimi niweze kujiondoa ili Yanga isonge mbele sababu pia tunamuhitaji GSM ni mtu ambaye ametusaidia sana”
Tukukumbushe tu Shija Richard ambaye amejiuzulu leo kwenye kikao cha kamati ya utendaji, alikuwa mjumbe wa kuteuliwa na mwenyekiti wa Yanga Dr Mshindo Msolla, Shija pia aliwa aliwahi kugombea nafasi ya Urais wa TFF.