MASHINDANO YA TOKYO OLYMPIC 2020 KUSIMAMA MPAKA MWAKANI
Ikiwa ni miaka 124 tokea michezo ya Olympic kuahirishwa, mara ya mwisho ikifutwa mwaka 1916, 1940 na 1944 yote kwa pamoja kutokana na vita ya kwanza nay a pii ya dunia. Safari hii kamati ya Olympic (IOC) imedhibitisha kufikia maamuzi ya kuahirisha mashindano haya ya Tokyo Olympic2020 yaliyokuwa yafanyike Julai 24 mwaka huu na sasa kuyasogeza mbele hadi majira ya joto hapo mwakani.
Katika tamko la pamoja waandaaji wa Tokyo2020 na IOC wamesema “Hali isyo ya kawaida wala kutabirika ya kuenea kwa virusi vya Corona, imepeekea taharuki sehemu mbalimbali duniani.
Kwa hali ya sasa kukiwa na kesi zaidi ya waadhirika 375,000 duniani na namba ikiongezeka kila saa na kulingana na taarifa zilizotolea na WHO, rais wa ICO na Waziri Mkuu wa Japan wameafiki kusogezwa mbele kwa mashindano ya michezo ya Olympic 2020 hadi baada ya mwaka 2020 na kabla ya majira ya joto 2021 ikiwa ni katika kulinda afya za wanamichezo na wote watakaohusika na michezo hii na jumuiya nzima ya kimataifa.”
Tamko hili liliendelea mbele likisema “Pamoja na kuahirishwa kwa mashindano haya hadi mwaka 2021, mashindano haya ya yatabakia na jina hili hili la sasa la Olympic na Paralympic Games Tokyo 2020. Viongozi wamekubaliana kuwa michezo ya Olympic ingesimama kama ishara ya matumaini kwa dunia katika kipindi hiki kigumu na mwenge wa Olympic kuwa kama mwanga na hivyo mwenge huo kubakia nchini Japan.”