CAF IMEIPIGA FAINI ZAMBIA KISA MASHABIKI
Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limetangaza kukipiga faini chama cha soka Zambia (FAZ) kutokana na mashabiki wake kurusha vitu uwanjani wakati wa mchezo wa Zambia dhidi ya Zimbabwe.
Mchezo wa Kundi G dhidi ya timu hizo ambao ulikuwa wa kuwania kufuzu kucheza fainali za AFCON 2021 ulichezwa Novemba 19 2019 na Zambia wenyeji wakapoteza kwa kufungwa 2-1 katika Uwanja wa Mashujaa Zambia.
Kufuatia kitendo hicho cha mashabiki wa Zambia kurusha vitu uwanjani ikiwemo chupa za maji, CAF wameipiga faini FAZ ya dola za kimarekani $ 7,500 (Tsh milioni 17.2)