TIMU MBILI ZA LALIGA ZAKATAA VIFAA VYA KUPIMIA CORONA
Klabu ya Celta Vigo inakuwa klabu ya pili ya Ligi Kuu ya nchini Hispania LaLiga kukataa vifaa vya kupimia virusi vya corona baada ya Real Valladolid kukataa pia.
Timu hizo zimekataa vifaa hivyo na kueleza kuwa vipelekwe kwa watu wenye mahitaji navyo zaidi kuliko wao.
Celta na Valladolid wote walikubaliana kuhusiana na hilo kama sehemu ya kujitoa kwa jamii yao, LaLiga walitoa vifaa bure kwa klabu zote kwa ajili ya kuhakikisha wachezaji wa timu zote wanakuwa salama.