MORRISON AKANUSHA KUWA MBIONI KWENDA SIMBA SC
Mshambuliaji wa Yanga raia wa Ghana Benard Morrison amekanusha vikali taarifa za kuwa mbioni kujiunga na wpinzani wa Yanga ambao ni Simba SC.
Morrison ameweka wazi taarifa hizo baada ya hivi karibuni kuzika taarifa kuwa viongozi wa Simba SC wapo katika mazungumzo nao ya kumshawishi ajiunge na wanamaimbazi.
“Ningependa kuwashukuru mashabiki na kila mmoja ndani ya Yanga kwa kunikaribisha pia nimesikia hivi vitu lakini mimi nipo hapa kuichezea Yanga na nimesaini mkataba kwa hivyo ninachokifanya sasa ni kuweka malengo yangu na kuweka mkazo ili kuona namna gani naisaidia Yanga” alisema Morrison alipohojiwa na Azam TV