AZAM FC YAVUNJA KAMBI, YARUHUSU WAKIMATAIFA KUTEJEA KWAO
Klabu ya Azam FC leo kupitia kwa afisa habari wao mpya Thabit Zachari wametangaza kuvunja kambi ya timu zao zote.
Azam FC wamevunja kambi hiyo ikiwa ni siku moja imepita toka waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa atangaze kusimamisha shughuli zote za michezo nchini kwa siku 30 kama njia ya kudhibiti kuenea kwa kasi kwa virusi vya corona nchini.
Thabit ameeleza kuwa wachezaji wao wakimataifa wameruhusiwa kurejea nchini kwao wakati huu wa katazo la siku 30 hadi April 17.