NDAIRAGIJE ASHINDWA KUTAJA SABABU ZA MKUDE KUTOWASILI TAIFA STARS
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars anayejulikana kwa jina la Etienne Ndairagije rai wa Burundi leo amepata wakati mgumu kidogo kutoa ufafanuzi kuhusu Jonas Mkude.
Etienne alikuwa uwanja wa Taifa akiendelea na mazoezi na wachezaji waliopo kambini kujiandaa na fainali za CHAN 2020 zinazotarajia kufanyika nchini Cameron mwezi April.
Swali la waandishi lilikuwa kiungo wa Simba SC Jonas Mkude mbona hajawasili kambini kama ilivyokuwa kwa wenzake yuko wapi ana tatizo gani? Wachezaji wa Yanga walikuwa na ruhusa ya kuchelewa kwa sababu walikuwa Rungwa Lindi kucheza na Namungo Machi 15.
”Ambao hawajafika sio Jonas Mkude ni pamoja na wachezaji wa Yanga wote wengine wataingia leo jioni, tatizo la Jonas ni alisema anaenda Morogoro hatujawa na uhakika wapi na kwa nini hajafika tukijua kinachoendelea kuna msemaji atawapa taarifa mimi siwezi kuongea” alisema Etienne