CORONA YAVUNJA MICHUANO YA EURO 2020
Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeahirisha michuano ya Euro 2020 mpaka mwaka 2021 ili kuzipa muda ligi za barani Ulaya kukamilisha misimu yao kutokana uwepo wa virusi vya Corona.
Michuano hiyo ya Euro ilipangwa kuchezwa mwaka huu kuanzia Juni 12 mpaka Julai 11,2021 katika mataifa 12 tofauti ya barani Ulaya
Maamuzi haya ya kuahirisha michuano hii mwaka huu,imekuja baada ya UEFA kufanya mkutano wa memba wake 55, bodi ya chama cha vilabu vya Ulaya na bodi ya Ligi za Ulaya.
Ligi za ndani zilikuwa ziishe kabla ya michuano ya 2020 kuanza, ratiba zimeharibika baada ya mlipuko wa virusi vya Corona.
Shirika la Afya Dunia (WHO) linasema Ulaya sasa imekuwa ni kiini cha ugonjwa huo ambao umeanzia nchini China.