TFF YAMPIGA FAINI KOCHA WA AZAM FC
Mechi namba 260: Azam FC 2 VS Simba SC 3Kocha wa Klabu ya Azam FC Aristica Cioba ametozwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki Tano) kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika, huku Simba ikipata ushindi wa 3-2.Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni namba 41(12) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha, kwa sheria za VPL ni lazima kocha kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo.