BODI YA LIGI YATANGAZA ADHABU VPL
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Machi 10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;
Mechi namba 253: Mwadui FC 2 v Police Tanzania FC 1
Kocha Msaidizi wa Police Tanzania, Ally Mtuli anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi Neema Mwambashi na kumtolea matusi ya nguoni.
Mechi hiyo ilichezwa Machi 04, 2020 katika Uwanja wa Mwadui FC mjini Shinyanga.
Mechi namba 268: Lipuli Fc 3 vs Ndanda Fc 3
Mchezaji wa Klabu ya Lipuli Fc Seif Ng’ingo na Mchezaji wa Klabu ya Ndanda Abubakar Hashimu wamepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki tano)Kila mmoja na kufungiwa Mechi tatu kwa kosa la kufanya vitendo vyenye kuashiria imani za ushirikina na uchawi hadharani, katika mechi iliyochezwa Machi 04,2020 katika uwanja wa Samora Iringa.