ASTON VILLA WAGAWA CHAKULA KWA SABABU YA CORONA
Klabu ya Aston Villa kupitia Aston Villa Foundation imeamua kukigawa chakula chao walichokuwa wameendaa kula kabla ya mechi dhidi ya Chelsea kwa mashirika ya watu wasio na makazi.
Mechi ya Aston Villa na Chelsea iliyokuwa ipigwe kesho Villa Park,haitochezwa baada ya ligi kuu nchini England kusimama mpaka April 04 kwa sababu ya virusi vya Corona.
Wakati huo huo Villa wamewashauri wachezaji wao kujizuia kupiga picha za Selfie na mashabiki na pia kuwazuia kusaini sahihi kwa mashabiki ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi.