SIMBA SC WAMEIMALIZA AZAM FC WANAISUBIRI YANGA
Simba SC leo wamecheza mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC n akuifunga kwa mabao 3-2 uwanja wa Taifa
Ushindi wa Simba SC kwa magoli ya Erasto Nyoni dakika ya 9, Deogratus Kanda dakika ya 16 na Meddie Kagere dakika ya 72 yanatafsirika kama salamu kwa watani zao wa jadi Yanga watakaocheza nao Machi 8.
Azam FC walipata mabao kupita Tigere dakika ya 5 na Iddi Nado dakika ya 50 kabla a Kagere kuzima ndoto za Azam FC za kuondoka na walau hata alama moja.