CRISTIANO RONALDO AFUNGUKA KUHUSU HALI YA MAMA YAKE
Staa wa soka Ulimwenguni Dunia Cristiano Ronaldo amethibitisha kuwa mama yake mzazi anaendelea vizuri kwa sasa baada ya kuumwa (ischemic stroke) na kukimbizwa na kulazwa Hospitali huko Madeira.
Katika taarifa aliyotoa Ronaldo jana usiku ilisema : “ Ahsante wote kwa meseji zenu za ‘support’ kwa mama yangu
“Kwa sasa yupo imara na anapata nafuu Hospital.
“Mimi na familia yangu tungependa kushukuru timu ya matibabu kwa kumuangalia”
Ischemi stroke husababishwa na damu kuganda ambayo hupelekea kuzuia au kuziba mishipa ya damu katika ubongo.
“Tunaweza kuthibitisha kulazwa kwa Doleres Aveiro (Mama yake Ronaldo) katika saa za mapema Machi 3 kwa ischemic stroke…” —Taarifa ya kituo cha Afya cha Madeira ilisema hivyo.
Baada ya kushuka kwenye ndege yake Binafsi hapo mjini Madeira, Ronaldo pamoja na mpenzi wake Georgina Rodriguez na mwanae mkubwa Cristiano Ronaldo Jr, walielekea katika hospitali hiyo aliyolazwa mama yake.