JERRY MURO AMPONDA YIKPE WAZIWAZI NA KUMSHUSHA EYMAEL
Afisa habari wa zamani wa Yanga Jerry Muro leo alikuwa mgeni katika mahojiano maalum na Wasafi FM kuhusiana na mwenendowa klabu yao.
Jerry ambaye amerudi kuhamasisha timu yake ifanye vizuri baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo hasi, amemkosa kocha wa Yanga Luc Eymael na kueleza sio bora kumshinda Mkwasa ambaye ni msaidizi wa Eymael.
“Kwangu mimi Mkwasa ni bora kuliko mzungu wenu (Luc Eymael). we unamuingiza Yikpe, unamuacha Mrisho Ngasa. Yani unajua kabisa huyu jamaa (Yikpe) ni boya na bado unamuingiza boya huyo huyo” Jerry Muro
Kwa sasa Jerry ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arumeru yupo Dar es Salaam likizo, ila ameamua kuhamasisha mashabiki kwenda uwanjani katika mchezo wa Yanga wa ASFC dhidi ya Gwambina leo uwanja wa Uhuru.