DEONTAY WILDER ATUPA LAWAMA KWA VAZI LAKE
Bondia Deontay Wilder amesema kuwa uzito wa nguo zake alizoingia nazo ulingoni ulipelekea kupigwa na Tyson Fury katika pambano lao lililopigwa na MGM Grand, Las Vegas Marekani juzi Februari 23
Wilder anasema mavazi hayo aliyoyavaa yalikuwa mazito sana na kusababisha miguu yake kutokuwa imara tangu mwanzo wa pambano.
“Hakuniumiza kabisa, bali ukweli ni kuwa mavazi yangu yalikuwa mazito sana,” Wilder alisema akihojiwa na Yahoo Sports.
“Sikuwa na miguu tangu mwanzo wa pambano. Katika raundi ya tatu,miguu yangu ilikuwa haipo sawa kabisa. Lakini mimi ni shujaa na watu wanajua kuwa mimi ni shujaa.”
Wilder,34, anasema alilijaribu kuvaa vazi hilo usiku mmoja kabla ya pambano lakini hakudhani kama linaenda kuwa zito kiasi hicho. “ Lilikuwa na uzito wa kilo 18, pamoja na Helmet na betri zote” alisema
Hili lilikuwa pambano lake la kwanza kupoteza Wilder. Na sasa amesema kuwa lazima warudiane kwa mara ya tatu.