DE BRUYNE AITAKA KLABU BINGWA ULAYA
Nyota wa Man City Kevin De Bruyne anaamini timu yao watahesabika wameshindwa kama hawataweza kuchukua kombe la klabu bingwa Ulaya msimu huu.
Kikosi cha Pep Guardiola kilishinda vikombe vyote nchini England msimu jana lakini hawakufurukuta barani Ulaya wakitolewa na Spurs katika hatua ya robo fainali.
“Kama hatutashinda (Klabu Bingwa) kila mtu atasema tumefeli kama miaka mitano iliyopita” —De Bruyne aliiambia Telegraph.
“Ni kitu ambacho hatujashinda bado. Siku zote tunataka kushinda kila kitu lakini wakati mwingine timu nyingine ni bora au wanacheza vizuri—kama Liverpool wanavyofanya msimu huu.”
Man City kesho wanaenda kujiuliza tena kwenye michuano hiyo ambapo watacheza na Real Madrid katika hatua ya 16 bora. Mechi hiyo itapigwa Santiago Bernabeu kabla ya marudiano Machi 17 nchini England.