WILLIAN APATA URAIA WA UINGEREZA
Mchezaji wa klabu ya Chelsea Willian Borges amesema amefaulu mtihani wa Uraia wa Uingereza baada ya kufeli miwili aliyofanya awali, na sasa amepata Uraia wa Uingereza
Mbrazil huyo,31,amebakisha muda wa miezi sita katika mkataba wake na klabu ya Chelsea lakini yeye pamoja na familia yake wanataka kuendelea kuishi London
“Kama utamuuliza mke wangu kama anataka kuondoka London, atasema hapana. Mabinti zangu ni hivyo hivyo. Kweli, Brazil ni Brazil,sawa? Ni nyumbani kwetu , utamaduni wetu. Huwa tunajihisi vizuri pale tunapoenda likizo na kuona familia na marafiki. Lakini London ni nyumbani kwangu kwa pili” alisema Willian katika mahojiano na The Players’ Tribune
Willian ameanza kuishi katika jiji la London tangu mwaka 2013 alipojiunga na klabu ya Chelsea akitokea Anzi Makhachakala ya Urusi.
“Hivi karibuni nimefaulu mtihani wa Uraia wa Uingereza. Ulikuwa mgumu. Historia ya Uingereza kwa kifupi: Miaka ya 1500, Miaka ya 1600, vita, mapambano,viongozi wakubwa, vitu kama hivyo.
“Maswali mengine ni magumu hata rafiki zangu wengine Waingereza hawajui majibu…”
“Nilifeli mitihani miwili ya kwanza, lakini nimefaulu wa tatu. Sasa ni raia wa Uingereza! Kwa hiyo London ndio sehemu ninataka kuishi. Ndipo nilipo na familia yangu,kanisa langu. Ninataka mabinti zangu wakue hapa.”
Kuwasili kwa Hakim Ziyech katika majira ya kiangazi mwaka huu kumeibua maswali mengi kuhusu Mustakabali wa Willian katika timu hiyo ambayo imekuwa ni ngumu kutoa mkataba mkubwa kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30.