PEP GUARDIOLA AMUONYA RAIS WA BARCA KUFURAHIA KUFUNGIWA KWAO
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amemjibu Rais wa klabu ya Barcelona Jose Maria Bartomeu ambaye amelipongeza shirikisho la soka la Ulaya UEFA kwa adhabu ya kuifungia Man City kufuatia kuvunja sheria ya matumizi ya fedha “Financial Fair Play”
Bartomeu aliwapongeza UEFA Jumanne ya wiki hii kwa kutoa adhabu hiyo ambapo Man City wamefungiwa kushiriki michuano ya Ulaya kwa misimu miwili ijayo.
“Ningependa kuwashukuru UEFA kuhusu Financial Fair Play,” alisema Bartomeu katika tuzo za waandishi wa habari ziitwazo
XIV Vazquez Montalban International Journalism Awards
“(UEFA) wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika miaka kadhaa iliyopita. Tumekuwa na uchunguzi mara kwa mara na tunawapa ushirikiano UEFA katika kila kitu wanafanya katika soka.”
Alisema Rais huyo wa klabu ya Barcelona ambayo Pep Guardiola aliipa ubingwa mara mbili wa klabu bingwa Ulaya alipokuwa akiifundisha kati ya mwaka 2008 na 2012
Maneno hayo ya Bartomeu hayakupokelewa vizuri na Pep Guardiola ambaye baada ya ushindi wake dhidi ya West Ham jana, aliamua kusafisha koo lake kwa kumjibu Rais huyo wa Barca
“Sijui kama (Barcelona) wananipeleleza lakini wananijua mimi, si muhimu kunipeleleza mimi.
“Kama wana furaha tumesimamishwa, ninamwambia Rais wa Barcelona,acha tukate furaha.
“Watu (wa Man City) sasa hivi wanaamini kile walichofanya. Tunaenda kukata rufaa…..lakini msiongee sana Barcelona”
“Huo ni ushauri wangu kwa sababu kila mmoja wakati mwingine huwa anahusika katika mazingira haya. Tunaenda kukata rufaa na tunatumaini mbeleni tunaweza kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Barcelona” alisema Kocha huyo.