HAJI MNOGA ATAMANI KUICHEZEA TANZANIA
Baba mzazi wa mchezaji wa klabu ya Portsmouth ya England Haji Mnoga, Mzee Mnoga ameeleza kuwa mwanae Haji anatamani kuitwa kucheza timu za taifa za vijana za Tanzania kabla ya kufikia maamuzi ya kuchagua kucheza timu ya taifa ya wakubwa.
Haji Mnoga kwa sasa ana uraia wa nchi mbili England na Tanzania kutokana na kuwa na umri chini ya miaka 18 na tayari ameshachezea timu ya taifa ya vijana ya England hivyo akifikia umri wa miaka 18 atatakiwa kuamua upande mmoja kuwa raia kamili wa Tanzani iili acheze timu ya taifa ya Tanzania au England kutokana na Tanzania kutoruhusu uraia wa nchi mbili.
Hivyo mzee Mnoga kupitia taarifa iliyotolewa katika ukurasa rasmi wa twitter wa mchambuzi wa Clouds FM Shaffih Dauda anaamini kija wake kabla ya kufanya maamuzi hayo atahitaji kuitwa kwanza timu za vijana.
“Mwanangu anatamani kucheza timu za vijana za Tanzania kwanza Kabla ya timu ya wakubwa. Nimeongea na viongozi wa soka Tanzania lakini bado hawajanipa mrejesho wa kueleweka kama watamwita ama lah” – Mzee Mnoga