MANARA ATETEA HOJA YA SAMATTA JUU YA MANENO MAKALI MTANDAONI
Watanzania mbalimbali wametoa mawazo yao kuhusiana na ombi la nahodha wa Tanzania anayekipiga England katika klabu ya Aston Villa Mbwana Samatta kuwa watanzania waache kutoa comment zenye matusi na zenye mlengo wa kueneza chuki miongoni mwao.
“Mashabiki wa soka Tanzania nafaham kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vzr ktk timu yangu mpya,lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mlengo mbaya katika ac/ za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi”
Leo afisa habari wa Simba SC licha ya baadhi ya watanzania kumjibu Samatta kwa kumwambia kuwa aachane na maneno ya mtandao afanye kazi yake, Haji Manara ambaye ni afisa habari wa Simba SC amekuwa na mawazo tofauti na kueleza kuwa tunamuharibia Samatta kwa wanaoandika mambo mabaya kuhusiana na Samatta.
“Ujinga tu kuamini kuwa yule mchezaji (Grealish) hampi pasi Samatta, Grealish ni mchezaji mkubwa sana captain wa timu, Samatta ndio kwanza amecheza mechi mbili hajazoea hana hata wiki mbili wale wachezaji wenzie lazima waone mikimbio yake jinsi anavyojiweka kwenye space wanaolalamika kuwa hampi pasi kwa hiyo nyine ndio mnampenda sana Samatta kuliko Aston Villa waliomsajili”
“Yaani timu itoe milioni 10 pauni za Uingereza iwe haimtakii mema sie huku nyumbani kwa sababu ya ushabiki mandazi ndio tunampenda sana Samatta, ten milioni imewekwa hela za kizungu sio hela zetu, shida moja watanzania tunaitumia vibaya mitandao ya kijamii tushazoea kutukana tutukaneni sisi majalala yenu mnaotutukana kila siku tuendeleeni kututukana lakini wale wazungu wa watu abuse ni mbaya sana in europe”