SOFIA KENIN AMTUPA NJE ASHLEING BARTY NA KUTINGA FAINALI
Sofia Kenin, 21, aliyepo katika nafasi ya 14 amemshangaza mchezaji namba 1 kwa ubora duniani, mwanadada Ashleing Barty kwa kumfunga kwa seti mfululizo 7-6 (8-6) 7-5.
Matokeo haya yameondoa ndoto ya Ashleing kuwa mwanadada wa kwanza M-australia kufika fainali za Australian Open baada ya miaka 40 huku ikiwa ni fainali ya kwanza ya Grand Slam kwa mwanadada Sofia Kenin.
Kenin sasa atakutana na bingwa wa Grand Slam mbili Mhispania Gabrine Muguruza aliyemtoa Simona Halep.