NOVAK DJOKOVIC AMTUPA NJE ROGER FEDERER AKITAFUTA FIKIA REKODI YAKE
Bingwa mtetezi wa Australian Open Mserbia Novak Djokovik amefanikiwa jiweka katika nafasi ya kutetea ubingwa wake baada ya kumtoa nyota mwenzake Mswiss Roger Federer kwa jumla ya seti 7-6 (7-1) 6-4 6-3.
Hii ilikuwa mechi ya 50 kati ya nyota hawa huku Djokovik akiwa anaongoza kwa ushindi 27 kwa 23.
Kulikuwa na uvumi wa Roger Federer kutoweza kutokea uwanjani kutokana na jeraha la sehemu ya paja lililomsumbua katika mechi iliyopita ila haikuwa hivyo kwani nyota huyo alitokea uwanjani na kuanza mchezo kwa kasi akiwa mbele kwa point 4 – 1 katika seti ya kwanza kabla ya Novak kurudi na kufaanya vyema.
Novak amefungwa mechi 3 tu katika mashindano 10 ya Australian Open akielekea kuchukua ubingwa wa huu kwa mara ya 8 na Grand Slam yake ya 17 ikiwa ni katika kuikimbiza rekodi ya Roger Federer ya muda wote ya mataji 20 ya Grand Slam.