MUGURUZA ATINGA FAINALI AKIMTOA SIMONA HALEP
Mhispania Gabrine Muguruza amefanikiwa ingia fainali ya Australian Open baada ya kumtoa Mromania Simona Halep aliyepo katika nafasi ya nne kwa jumla ya seti 7-6 (10-8) 7-5. Hii ni fainali ya kwanza kwa bingwa huyu wa Grand Slam mara mbili tokea alipochukua taji la Wimbledon mwaka 2017.
Muguruza sasa atakutana na Mmarekani Sofia Kenin aliyemtoa nyota Ashleing Barty.