ZVEREV AMFUNGA STAN WAWRINKA NA KUFIKA NUSU FAINALI AUSTRALIAN OPE
Alexandrer Zverev, 22, amefanikiwa ingia nusu fainali yake ya kwanza ya Grand Slam baada ya kumfunga Stan Wawrinka, 34, kwa seti 1-6 6-3 6-4 6-2 akipoteza seti kwa mara ya kwanza katika mashindano haya.
Sasa atakutana na mshindi wa mechi ya Rafael Nadal dhidi ya Dominic Thiem. Wawrinka sasa anakuwa ametolewa kwenye hatua ya robo fainali kwa mara ya tatu katika Grand Slam 4 zilizopita