OLE: SANCHEZ ATARUDI NA KUWADHIBITISHIA MLIKOSEA
Mchezaji Alexis Sanchez atarejea katika klabu yake ya Manchester United baada ya kuitumikia klabu ya Inter kwa mkopo msimu mzima.
Hili limethibitishwa na kocha wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer aliyeongeza kuwa “Alexis atarudi majira ya joto na kuwathibitishia wote kuwa mlikosea”
Sanchez alijiunga na Man United January 2018 na kufankiwa kufunga magoli 5 katika mechi 45, akilipwa mshahra wa takribani pauni 400,000 (takribani shilling billion 1) kwa wiki ukiwa ndio mkubwa kuliko mchezaji mwingine yeyeote Man United.
Mchezaji huyo amesema hana chochote anachojutia kujiunga na Manchester United, amecheza mechi 7 tu za Serie A msimu huu na kufunga goli moja huku akikaa nje muda mwingi kutokana na majeraha.