DOMINIC THIEM AMTUPA NJE RAFAEL NADAL AUSTRALIAN OPEN
Mchezaji namba moja kwa ubora duniani Rafael Nadal ameshindwa songa mbele nusu fainali ya Australia Open baada ya Mhispania Dominic Thiem, 26, aliyepo katika nafasi ya 5 kufanikiwa mfunga kwa jumla ya seti 7-6 (7-3) 7-6 (7-4) 4-6 7-6 (8-6)
Mhispania huyu sasa atakutana na Mjerumani Alexander Zverev siku ya Ijumaa katika nusu fainali itakayokuwa ya kwanza kwa wachezaji hawa wawili na mshindi atakutana na mshindi katika mechi ya nyota Roger Federer dhidi ya bingwa mtetezi Novak Djokovic.
“Ulikuwa wakati wa kipekee kwangu kufanikiwa mtoa Rafa na kusonga mbele nusu fainali. Nilipata wakati mgumu lakini niliweza badilisha.” Alisema Thiem ambaye amekuwa akichukuliwa kama moja ya Vijana walio na uwezo wa kushindana na wachezaji nyota watatu wakubwa. (Roger Federer, Rafael Nadal na Novak Djokovic)
Matokeo haya yanamfanya Nadal asubirie mashindano mengine ili ajaribu ifikia rekodi ya muda wote ya Roger Federer ya kutwaa mataji 20 ya Grand Slam’