ARSENAL KUMCHUKUA PABLO MARI KWA MKOPO
Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano ya kumchukua mchezaji Pablo Mari kwa mkopo wa miezi 6 kwa makubaliano ya kumchukua moja kwa moja majira ya joto. Klabu ya Flamengo ilimtangaza beki Leo Pereira tokea Athletico Paranaense kama mridhi wa Pablo siku ya Jumanne.
Mari alikwisha safari kwenda London mara ya kwanza kukamilisha usajili kabla ya Flamengo kukataa kwa maelezo kuwa klabu ya Arsenal ilileta mapendekezo mapya ya usajili huo dakika za mwisho. Hata hivyo safari hii usajili huu unatarajiwa kamilika kabla ya siku ya Ijumaa.
Arsenal wanakabiliana na tatizo la safu ya ulinzi huku beki Shkodran Mustafi akiwa majeruhi akiungana na Calum Chambers, Kieran Tierney na Sead Kolasinac ambao wote nao ni majeruhi.