KLOPP AGOMA CHEZESHA KIKOSI CHA KWANZA MECHI YA MARUDIANO FA
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameseam hakuna mchezaji wa kikosi cha kwanza atajumuishwa katika mechi ya marudiano ya kombe la FA raundi ya 4 dhidi ya Shrewsbury Town mapema mwezi ujao kutokan na mapumziko ya majira ya baridi ya EPL.
Kikosi cha kocha huyo kililazimishwa kuwa na mechi ya marudiano na Shrewsbury Town baada ya kutoka sare ya goli 2 – 2, Klopp hajawahi ifikikisha Liverpool katika raundi ya 5 tokea atue katika kikosi hicho mwaka 2015 ila sasa anaonekana kutaka badili hali hii.
Akiongea na waandishi wa habari Klopp alisema
“Mwezi April 2019 tulipokea barua toka Premier League ikituomba kuheshimu mapumziko ya majira ya baridi na kutokuweka mechi ya kirafiki wala ya mashindano katika kipindi hiki. Nimeongea na Vijana wiki mbili zilizopita na nimewaambia watakuwa na mapumziko hayo, vijana wadogo ndio watakaocheza mechi hiyo sababu wengine watakuwa mapumziko.”
Amedhibitisha kuwa kocha wa kikosi cha vijana wa umri chini ya miaka 23 Neil Critchley ataongoza timu katika mechi hiyo. Critchley aliongoza kikosi cha Liverpool dhidi ya Aston Villa katika mechi ya Carabao robo fainali walipofungwa goli 5 – 0 kipindi timu ya wakubwa ilipokuwa nchini Quatar kushiriki michuano ya kombe la dunia ya vilabu.
Wachezaji wana familia na hawajawa na muda wa mapumziko hasa lwachezaji wa kimataifa kama Mo Salah, Virgil van Dijk, Wijnauldum na Sadio Mane. Wanahitaji kuwa na mapumziko, haiwezekani upande mmoja ukatuambia sio muhimu.